Mgeni wetu anaitwa Bi. Claudine Byamungu Nanjuchi. Yeye ndiye mratibu wa shirika la wanawake la Hope and Peace ambalo linafanya kampeni ya amani na mshikamano wa kijamii huko Kivu Kusini na hivi karibuni katika majimbo mengine mawili ya mashariki mwa nchi ambayo yametikiswa na migogoro ya kivita, ambayo ni Kivu Kaskazini na Ituri. Redio Okapi ilikutana naye kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wake wa miaka mitano siku ya sita tarehe tano Juni mwaka tunao huko Bukavu.